KISWAHILI Form 3 Topic 6

UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO
Misingi ya Kuandika Insha
Elezea misingi ya kuandika insha
Insha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni pamoja na matumizi ya tamathali za semi, misemo nahau, methali na taswira.
Muundo wa Insha
Kwa kawaida insha inakuwa na sehemu kuu nne: kichwa cha insha, utangulizi, kiini na hitimisho.
  1. Kichwa cha insha;Kichwa cha insha hudokeza kile utachokijadili katika insha yako, hubainisha wazo kuu la mada inayohusika. Kwa kawaida kichwa cha insha huandikwa kwa sentensi fupi. Mfano; maisha ya kijijini, mimba za utotoni.
  2. Utangulizi;Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako. Utangulizi unakuwa katika aya moja fupi.
  3. Kiini cha insha; Katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.
  4. Hitimisho; Hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichojadiliwa katika insha.
Insha za Kisanaa
Andika insha za kisanaa
Insha ya kisanaa ni ile inayotumia lugha ya kisanaa yaani yenye tamathali za semi kama vile sitiari, tashbiha, taniaba na mubalagha. Aidha insha ya kisanaa hutumia mbinu nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, na tanakali sauti. Vilevile insha za kisanaa huwa na lugha zenye mvuto na misemo kama nahau, methali na tamathali za semi.
Activity 1
Andika insha za kisanaa

Tangazo ni taarifa za wazi zinazotoa ujumbe fulani kwa walengwa wanaohusika na ujumbe huo. Ujumbe unaweza kuwa na lengo la kushawishi, kuarifu, kuelekeza, na kadhalika.
Vipengele vya Kuzingatiwa katika Uandishi wa Mtangazo
Elezea vipengele vya kuzingatiwa katika uandishi wa matangazo
Malengo ya matangazo
  • Kutoa taarifa;Lengo mojawapo la matangazo ni kutoa taarifa, mfano wa matangazo yanayotoa taarifa ni mialiko, tangazo la kifo, alama za barabarani, matangazo ya kazi.
  • Kuonya; Matangazo pia yana lengo la kuonya, kwa mfano matangazo kama vile ya kutovuta sigara, UKIMWI na kadhalika.
  • Kushawishi; Matangazo pia yana lengo la kushawishi, matangazo yenye lengo hili mara nyingi ni matangazo ya biashara ambayo kwa kweli lengo lake ni kushawishi wateja ili wanunue bidhaa zao, mtangazo ya mialiko hasahasa ya tukio fulani, labda msanii anazindua albamu fulani na kadhalika.
Jinsi ya kuandika matangazo
Ili tangazo liweze kufanikisha kufikia lengo lililokusudiwa kuna mambo kadhaa ya kufanya; mambo hayo ni kama yafuatayo:
  • Kichwa cha habari; Mara nyingi matangazo yanakuwa na kichwa cha habari, hii inasaidia kujua kwa haraka kuwa tangazo linahusika na kitu gani.
  • Kuonesha aina ya bidhaa/huduma; Hiki ndicho kiini cha tangazo, hapa tangazo linaonesha ujumbe uliokusudiwa kufikishwa kwa wahusika, sasa ujumbe huu waweza kuwa ni bidhaa inayotangazwa au huduma inayotolewa au kazi inayotangazwa au mwaliko unahusu nini.
  • Anwani; Hapa tangazo linaonesha mahali ambapo watoa tangazo walipo, yaani ofisi zao zilipo ambapo wahusika wa tangazo wanaweza kwenda na kuwakuta. Kama ni tangazo la mwaliko basi ni lazima lionesha shughuli yenyewe itafanyika wapi.
  • Njia za mawasiliano; Kama ni tangazo la biashara au la kazi au la mwaliko ni muhimu kutoa mawasiliano. Mawasiliano hayo yanaweza kuwa ni namba ya simu, fax, wavuti (kwa taarifa zaidi), barua pepe.
Mbinu za uandishi wa matangazo
Ili tangazo liweze kuvuta umakini wa watu ni lazima liwe na mwonekanao fulani. Zifuatazo ni mbinu za uandishi wa matangazo.
  • Matumizi ya picha;Matangazo mengi ya biashara huwa yanaambatana na picha, picha hizi hujaribu kumshawishi mteja aamini kuwa ile bidhaa ni bora na hivyo ni muhimu kuwa nayo au kuinunua.
  • Maneno machache; Matangazo hutumia maneno machache kwa lengo la kutomchosha mlengwa lakini wakati huohuo maneno hayo yana nguvu ya kumshawishi mlengwa.
  • Lugha ya kisanii; Maneno ya kisanii katika matangazo huwa ni mepesi kukumbukwa na huwa yanaeleweka kirahisi. Kwa mfano, matumizi ya vivumishi, litakuwa ni bonge la shoo, njoo ujinunulie pamba za ukweli, n.k. Matumizi ya mubalagha, kwa mfano; mtandao unaoongoza Tanzania, mganga bingwa afrika mashariki na kati n.k
  • Matumizi ya watu maarufu;Matangazo mengi hususani ya biashara hupenda kutumia watu maarufu ili kuwashawishi walengwa. Kwa mfano kama ni tangazo juu ya bidhaa fulani, huweza kumwonesha pengine msanii maarufu, miss Tanzania, au mchezajia mpira maarufu. Sasa mlengwa anapoona kwamba hata mtu maarufu anatumia hiyo bidhaa, anashawishika na yeye kuitumia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Back to top button
Close

Adblock Detected

We've noticed that you're using an adblocker. Our website relies on ads to provide free content. Please consider disabling your adblocker support us. Thank you for your support.